Majuto ni mjukuu @Kenya

This blog is for people who do not have time to read long articles which go on forever.

Tuesday, June 05, 2007

Yote Yawezekani bila Uhuru Kenyatta na Moi

Wakenya wenzangu na hasa wanachama wa ODM_K wamepigwa na bumbwazi sanaa jinsi Uhuru Kenyatta analipepeta chama hilo, mara juu mara chini. Lugha kubwa atumiayo binadamu kuwasiliana na mwenziye haitumii sauti.Mara nyingi ujumbe unamfikia mtarajiwa kwa lugha ya mwili. Jinsi unavyokaa na mdau tu , anapata ujumbe kuwa unamfikiriaje
Jinsi unavyo mtazama tu yule kisura au rijali, anajua kuwa unamuhusudu au sivyo.Hivi ni rijali au lijari? Lakini nahisi unajua na maanisha nini.

Ingawa Uhuru Kenyatta hajasema kinaganaga ati halipendi chama cha ODM, lugha yake ya mwili ilisema hivyo zamani zakale. Kwa hivyo sisi kama wanachama wa ODM ni lazima tumchukulie hatua ya kumuondoa katika pati hili. Yaonekana kana kwamba anampigia debe "mmoja wao" yaani mzee Kibaki, kwa hivyo hakuna haji ya kumbebeleza tena. Huyu kijani ameonyesha alama ya udikteta. Mtoto wa nyoka ni nyoka. Mbona urafiki wake ni wa utata and utatizo. Wakati umefika, kumtupilia mbali Uhuru Kenyatta. Uhuru hatuongezei wala hatupunguzii. Nimenena

0 Comments:

Post a Comment

<< Home